Matayo 6

Kuwasaidia Maskini

1“Angalieni msitende mema mbele ya watu ili muonekane na watu. Kwa maana mkifanya hivyo hamtapata thawabu itokayo kwa Baba yenu aliye mbinguni. 2“Kwa hiyo mnapowasaidia maskini msitangaze kwa tarumbeta kama wafanyavyo wanafiki katika masinagogi na mitaani ili wasi fiwe na watu. Nawaambia wazi, wao wamekwisha pata tuzo yao. 3Lakini ninyi mnapotoa sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kulia unafanya nini; 4ili sadaka yako iwe ni siri. Naye Baba yako wa mbinguni anayeona sirini ata kupa thawabu.”

Mafundisho Kuhusu Sala

5“Na mnaposali, msiwe kama wanafiki; maana wao wanapenda kusimama na kusali katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Nawaambieni kweli, wao wamekwisha kupata tuzo yao. 6Unaposali, nenda chumbani kwako ufunge mlango na umwombe Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini atakupa tha wabu.

7“Mnaposali msirudie maneno yale yale kama wafanyavyo watu wa mataifa wasiomjua Mungu. Kwa maana wao hudhani kwamba watasi kilizwa kwa sababu ya wingi wa maneno yao. 8Msiwe kama wao, kwa sababu Baba yenu anajua mahitaji yenu hata kabla hamjaomba.” 9Basi msalipo ombeni hivi: ‘Baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe. 10Ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni. 11Utupatie leo riziki yetu ya kila siku. 12Na utusamehe makosa yetu kama sisi tulivyokwisha kuwa samehe waliotukosea. 13Na usitutie majaribuni, bali utuokoe kutokana na yule mwovu,’ [Kwa kuwa Ufalme na nguvu na utukufu ni vyako milele. Amina.] 14Kama mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe na ninyi; 15lakini msipowasamehe watu makosa yao, Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.

Mafundisho Kuhusu Kufunga

16“Mnapofunga, msionyeshe huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kujionyesha. Nawaambieni kweli kwamba wao wamekwisha kupata tuzo yao. 17Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kuosha nyuso zenu 18ili kufunga kwenu kusijulikane kwa mtu ila Baba yenu aliye sirini; na Baba yenu aonaye katika siri atawapa thawabu.” Akiba Ya Mbinguni. 19“Msijiwekee mali nyingi duniani ambapo wadudu na kutu huharibu na wezi huvunja na kuiba. 20Lakini jiwekeeni mali mbinguni ambapo wadudu na kutu hawaharibu na wezi hawavunji na kuiba. 21Kwa sababu pale akiba yako ilipo ndipo moyo wako uta kapokuwa.”

Jicho Ni Taa Ya Mwili

22“Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni zuri, mwili wako wote utakuwa na nuru. 23Lakini kama jicho lako ni bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Kwa hiyo kama nuru iliyomo ndani yako ni giza, hakika utakuwa na giza la kutisha.”

Mungu Na Mali

24“Hakuna mtu anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa sababu, ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au atamthami ni mmoja na kumdharau mwingine. Huwezi kumtumikia Mungu na mali.”

Msiwe Na Wasiwasi

25“Kwa hiyo nawaambia, msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini; au kuhusu miili yenu: mvae nini. Kwani maisha si zaidi ya chakula? Na mwili zaidi ya mavazi? 26Waangalieni ndege wa angani: wao hawapandi wala kuvuna wala kuweka cho chote ghalani. Lakini Baba yenu wa mbinguni anawali sha. Je ninyi, si wa thamani zaidi kuliko ndege? 27Ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi kwenye maisha yake?

28“Na kwa nini mnahangaikia mavazi? Angalieni maua ya mwi tuni yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayashoni nguo. 29Lakini nawaambia, hata mfalme Sulemani katika ufahari wake wote hakuwahi kuvikwa kama mojawapo la maua hayo. 30Lakini ikiwa Mungu anay avisha hivi maua ambayo leo yapo na kesho yanatupwa motoni, je, hatawavisha ninyi vizuri zaidi, enyi watu wenye imani haba? 31Kwa hiyo msiwe na wasiwasi mkisema, ‘Tutakula nini?’ au ‘Tutakunywa nini?’ au ‘Tutavaa nini?’ 32Mambo haya ndio yanay owahangaisha watu wa mataifa wasiomjua Mungu; na Baba yenu wa mbinguni anafahamu kwamba mnahitaji yote hayo. 33Lakini uta futeni kwanza Ufalme wa mbinguni na haki yake, na haya yote mtaongezewa. 34Kwa hiyo msihangaike kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajihangaikia yenyewe. Kila siku ina shida zake za kutosha.”