Neno La Uzima
1Tunawaandikieni kuhusu kile ambacho kimekuwapo tangu mwanzo, ambacho tumekisikia na kukiona kwa macho yetu; ambacho tumekigusa kwa mikono yetu; yaani Neno la uzima. 2Uzima huo uli tokea, nasi tumeuona na tunaushuhudia, na tunawatangazieni uzima wa milele uliokuwa kwa Baba, nao ukadhihirishwa kwetu. 3Tunawa tangazia hicho tulichokiona na kukisikia ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi. Na ushirika tulio nao ni wetu na Baba na Mwa nae Yesu Kristo. 4Tunawaandikieni mambo haya ili furaha yetu ikamilike.
Kutembea Nuruni
5Huu ndio ujumbe tuliousikia kutoka kwake, ambao tunawatan gazia: Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza kamwe. 6Tukisema tuna ushirika naye huku tunaendelea kuishi gizani tunasema uongo, wala hatutendi yaliyo ya kweli. 7Bali tukiishi nuruni, kama yeye alivyo nuru, tunakuwa na ushirika sisi kwa sisi na damu ya Mwanae Yesu, inatutakasa dhambi zote. 8Tukisema kwamba hatuna dhambi tunajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu. 9Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwa minifu na wa haki na atatusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote. 10Tukisema hatujatenda dhambi tunamfanya yeye kuwa mwongo, na neno lake halimo ndani yetu.