1Kutoka kwa Paulo, Silvano na Timotheo. Kwa kanisa la Wath esalonike mlio wa Mungu Baba yetu na wa Bwana Yesu Kristo. Tuna watakieni neema na amani.
Shukrani Kwa Imani Ya Wathesalonike
2Tunamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu wote na kuwaom bea pasipo kukoma. 3Tunakumbuka daima mbele za Mungu Baba yetu, kazi yenu inayotokana na imani, juhudi yenu kubwa katika upendo, na uvumilivu wenu unaotokana na tumaini mlilonalo kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 4Ndugu zetu mnaopendwa na Mungu, tunafahamu kwamba Mungu amewachagua 5kwa maana Injili yetu haikuwajia kwa maneno matupu bali ilidhihirishwa kwa nguvu na kwa Roho Mtakatifu, mkawa na uhakika kamili. Ninyi mnajua jinsi tulivyoishi pamoja nanyi kwa faida yenu. 6Nanyi mkatuiga sisi, mkamuiga na Bwana; kwa maana mlilipokea neno kwa furaha mliyopewa na Roho Mtakatifu ingawa mlipata mateso makali. 7Kwa hiyo mkawa kielelezo kwa waamini wote wa Makedonia na Akaya.
8Maana neno la Mungu limeenea kutoka kwenu, sio mpaka Make donia na Akaya tu, bali imani yenu kwa Mungu imejulika na mahali pote. Kwa hiyo hatuhitaji kusema lo lote kuhusu imani yenu; 9kwa maana wao wenyewe wanaeleza jinsi mlivyotupokea. Wanasimulia jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaacha ibada za sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai na wa kweli; 10na kumngoja Mwanae kutoka mbin guni, ambaye alimfufua kutoka kwa wafu, yaani Yesu. Yeye anatu komboa kutoka katika ghadhabu ijayo.