Wagalatia 1

1Kutoka kwa Paulo, mtume niliyetumwa, si kutoka kwa watu wala sikuchaguliwa na mwanadamu, bali nimetumwa na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu. 20 Nawahakikishieni mbele za Mungu kuwa ninayowaandikieni si uongo.

3Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, 4ambaye alijitoa kwa ajili ya dhambi zetu ili apate kutuokoa kutoka katika nyakati hizi za uovu. 5Yeye apewe utukufu milele na milele. Amina.

6Nashangaa kuona kwamba mnamwacha upesi hivyo yule aliye waita kwa neema ya Kristo mkaanza kufuata Injili nyingine. 7Ukweli ni kwamba hakuna Injili nyingine, ila nafahamu kuwa wako watu wanaowavuruga, ambao wanataka kuipotosha Injili ya Kristo. 8Lakini hata ikiwa ni sisi au ni malaika atokaye mbinguni, kama mtu akiwahubiria Injili ambayo ni tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi mtu huyo na alaaniwe. 9Kama tulivyokwisha sema kabla, sasa nasema tena, kwamba mtu ye yote atakayewahubiria Injili tofauti na ile mliyokwishaipokea, basi mtu huyo na alaaniwe.

10Je, sasa mimi nataka nipate upendeleo kutoka kwa bina damu au kutoka kwa Mungu? Au nataka niwapendeze watu? Kama ningekuwa najaribu kuwapendeza watu, nisingekuwa mtumishi wa

Wito Wa Paulo

11Ndugu zangu, napenda mfahamu kwamba Injili niliyo wahubi ria siyo Injili ya binadamu. 12Kwa maana mimi sikuipokea Injili kutoka kwa binadamu, wala sikufundishwa na mtu, bali nili pata mafunuo moja kwa moja kutoka kwa Yesu Kristo. 13Ninyi mmekwisha sikia juu ya maisha yangu ya zamani nilipokuwa katika dini ya Kiyahudi; jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungu na kujaribu kuliangamiza. 14Nami niliwashinda wengi miongoni mwa Wayahudi wenzangu kwa maana nilikuwa nimejawa na juhudi ya kushika mapo keo ya baba zetu. 15Lakini yeye aliyenichagua hata kabla sijazaliwa na akaniita kwa neema yake, 16alipopenda kumdhihiri sha Mwanae kwangu ili nimhubiri miongoni mwa watu wa mataifa, sikushauriana na mtu ye yote. 17Sikwenda kwanza Yerusalemu kuonana na wale waliokuwa mitume kabla yangu, bali nilikwenda Arabuni, ndipo nikarudi Dameski. 18Kisha baada ya miaka mitatu nilikwenda Yerusalemu kuo nana na Kefa na nilikaa naye siku kumi na tano. 19Lakini siku waona wale mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. 21Baadaye nilikwenda sehemu za Siria na Kilikia. 22Lakini mimi binafsi sikujulikana kwa wakristo wa makanisa ya huko Uyahudi. 23Ila walisikia wengine wakisema, “Yule mtu ambaye zamani alikuwa akitutesa sasa anahubiri imani ile ile aliyokuwa akitaka kuiangamiza.” 24Kwa hiyo wakamtukuza Mungu kwa sababu yangu.