Bwana Atakuja Ghafla
1Basi, ndugu wapendwa, hatuna haja ya kuwaandikieni kuhusu nyakati na tarehe atakayokuja Bwana, 2kwa maana mnajua wazi kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi anavyokuja usiku. 3Wakati watu bado wanasema, “Kuna amani na usalama’
4Bali ninyi, ndugu wapendwa, hamko gizani kuhusu mambo haya hata siku ile iwashtue kama mwizi. 5Ninyi nyote ni wana wa nuru, wana wa mchana. Sisi sio watu wa giza au wa usiku. 6Kwa hiyo basi, tusiwe kama baadhi ya watu wengine, waliolala, bali tukeshe na kuwa na kiasi. 7Maana wale wanaolala hulala usiku, na wale wanaolewa hulewa usiku. 8Lakini kwa kuwa sisi ni watu wa mchana, basi tuwe na kiasi, tukivaa imani na upendo kama kinga ya kifuani na kuvaa tumaini letu la wokovu kama kofia ya chuma. 9Maana Mungu hakutuchagua ili tupate ghadhabu yake bali tupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. 10Yeye alitufia ili kama tuko hai au hata kama tumekufa, tuishi pamoja naye. 11Kwa hiyo farijianeni na kujengana kama mnavyofanya sasa.
Maagizo Ya Mwisho Na Salamu
12Sasa tunawaomba, ndugu wapendwa, muwaheshimu wale wanaofanya kazi kwa bidii miongoni mwenu; ambao wana mamlaka juu yenu katika Bwana na ambao wanawaonya. 13Wapeni heshima kubwa na kuwapenda kwa ajili ya kazi yao. Ishini kwa amani kati yenu. 14Na tunawasihi, ndugu wapendwa, muwaonye wale walio wavivu, watieni moyo walio waoga, wasaidieni walio dhaifu na muwe na subira na kila mtu. 15Hakikisheni kuwa mtu hamlipi mwenzake ovu kwa ovu bali daima jitahidini kutendeana wema ninyi kwa ninyi na watu wengine wote.
16Furahini wakati wote, 17ombeni pasipo kukoma, 18shu kuruni katika kila hali; kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu mkiwa ndani ya Kristo Yesu. 19Msiuzime moto wa Roho Mtakatifu; 20msidharau unabii. 21Pimeni kila kitu. Yash ikeni kwa makini yaliyo mema. 22Epukeni uovu wa kila namna.
23Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase kabisa. Roho zenu, nafsi zenu na miili yenu na ihifadhiwe bila kuwa na lawama kwa wakati atakapokuja Bwana wetu Yesu Kristo. 24Yeye aliyew aita ni mwaminifu naye atafanya haya.
25Ndugu wapendwa, tuombeeni. 26Wasalimieni ndugu wote kwa busu takatifu. 27Nawaagizeni mbele za Bwana mhakikishe kuwa ndugu wote wanasomewa barua hii.