Yesu Ajaribiwa Na Shetani
1Kisha Yesu akaongozwa na Roho Mtakatifu mpaka nyikani ili akajaribiwe na shetani. 2Akakaa huko siku arobaini akifunga, pasipo kula kitu cho chote mchana na usiku, hatimaye akaona njaa. 3Ndipo shetani akamjia akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”
Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”
4Lakini Yesu akamjibu, “Imeandikwa, ‘Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno analotamka Mungu.’ ”
5Ndipo shetani akampeleka Yesu mpaka mji mtakatifu wa Yerus alemu, akamweka juu ya mnara wa Hekalu, 6akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa kuwa imeandikwa, ‘Atawaagiza malaika wake wakuhudumie,’ na, ‘Watakuinua juu mikononi mwao ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe.’ ”
7Yesu akamjibu, “Pia imeandikwa, ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’ ”
8Kwa mara nyingine shetani akamchukua Yesu mpaka kwenye kilele cha mlima mrefu akamwonyesha milki zote za dunia na fahari zake, 9kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote kama ukipiga magoti na kuniabudu.”
10Yesu akamwambia, “Ondoka hapa shetani! Kwa maana imean dikwa, ‘Utamwabudu Bwana Mungu wako na utamtumikia yeye peke yake.’ ” 11Ndipo shetani akamwacha, na malaika wakaja wakamhu dumia.
Yesu Aanza Kuhubiri
12Yesu aliposikia kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ameka matwa na kuwekwa gerezani, alirudi Galilaya. 13Akaondoka Nazareti akaenda kuishi Kapernaumu karibu na ziwa, katika eneo la Zabuloni na Naftali. 14Utabiri wa nabii Isaya ukatimia, kama alivyosema: 15“Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini, ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya watu wa mataifa - 16watu wale waishio katika giza wameona nuru kuu; na kwa wale wanaoishi katika nchi ya giza la mauti, nuru imewaangazia.” 17Tangu wakati huo, Yesu alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana Ufalme wa mbinguni umekaribia.”
Yesu Awaita Wanafunzi Wanne
18Yesu alipokuwa akitembea kando kando ya ziwa la Galilaya aliwaona ndugu wawili, Simoni ambaye aliitwa Petro na Andrea ndugu yake. Walikuwa katika mashua wakitupa nyavu zao baharini kwa maana wao walikuwa wavuvi.
19Yesu akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya muwe wavuvi wa watu.” 20Wakaziacha nyavu zao mara moja, wakamfuata.
21Alipoendelea mbele kidogo, aliwakuta ndugu wengine wawili, Yakobo na Yohana, wakiwa wamekaa kwenye mashua pamoja na baba yao Zebedayo wakishona nyavu zao; akawaita. 22Wakaacha nyavu zao mara moja, wakamfuata.
Yesu Ahubiri Na Kuponya Wagonjwa
23Yesu alizunguka Galilaya yote, akifundisha katika masi nagogi na kuhubiri Habari Njema ya Ufalme wa mbinguni, na kupo nya kila ugonjwa na kila udhaifu. 24Kwa hiyo sifa zake zilienea sehemu zote za Siria. Nao wakamletea wagonjwa wote, waliosumbu liwa na maradhi mbalimbali na maumivu, watu waliopagawa na mashe tani, wenye kifafa na waliopooza, naye akawaponya.
25Umati mkubwa wa watu ukamfuata kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Yudea na kutoka ng’ambo ya mto Yordani.