Matayo 15

Mafundisho Ya Mafarisayo

1Baadhi ya walimu wa sheria na Mafarisayo kutoka Yerusalemu walikuja kwa Yesu wakamwuliza, 2“Mbona wanafunzi wako hawafu ati mafundisho ya wazee wetu? Kwa maana wao hawanawi mikono ka bla ya kula!” 3Yesu akawajibu, “Mbona ninyi mnazivunja amri za Mungu kwa ajili ya mafundisho yenu? 4Kwa maana Mungu alisema: ‘Waheshimu baba yako na mama yako’ na ‘Ye yote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’ 5Lakini ninyi mnasema kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kuku saidia nacho nimekitoa kwa Mungu,’ basi hana wajibu tena wa kum saidia baba yake. 6Basi kwa ajili ya mafundisho yenu mnavunja amri ya Mungu. 7Ninyi wanafiki! Isaya alisema sawa juu yenu alipotabiri kwamba: 8‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami. 9Kuniabudu kwao ni bure, na mafundisho yao ni maagizo ya wanadamu.’ ”

Usafi Wa Kweli

10Yesu akaita ule umati wa watu akawaambia, “Sikilizeni kwa makini na mwelewe: 11kinachomfanya mtu kuwa mchafu mbele ya Mungu si kile kiingiacho kinywani mwake, bali ni kile kitokacho kinywani mwake.” 12Kisha wanafunzi wake wakaja wakamwambia, “Unafahamu kwamba Mafarisayo walichukizwa sana na yale maneno uliyosema?”

13Akawajibu, “Kila mmea ambao Baba yangu wa mbinguni hakuupanda, utang’olewa. 14Waacheni; wao ni viongozi vipofu. Na kama kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, wote wawili watatumbukia shimoni.”

15Petro akasema, “Tuambie maana ya mfano huo.” 16Yesu akawauliza, “Hata na ninyi bado hamwelewi? 17Hamtambui kwamba cho chote kiingiacho mdomoni hupitia tumboni na hatimaye hutolewa nje? 18Lakini kitokacho kinywani hutoka moyoni, na hiki ndicho kinachomfanya mtu kuwa mchafu. 19Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo machafu, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na matukano. 20Haya ndio yamchafuayo mtu, lakini kula bila kunawa mikono hakumchafui mtu.”

21Na Yesu akaondoka mahali hapo akaenda sehemu za Tiro na Sidoni. 22Mwanamke mmoja Mkanaani aliyeishi sehemu hizo akaja kwake, akamlilia, akasema, “Nihurumie, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa na pepo na anasumbuka sana.” 23Lakini Yesu hakumjibu neno. Basi wanafunzi wake wakamwendea wakamwomba, “Mwambie aende zake, kwa maana anaendelea kutupigia kelele. ” 24Akajibu, “Nimetumwa tu kwa ajili ya kondoo wa Israeli wal iopotea.”

25Lakini yule mwanamke akaja, akapiga magoti mbele ya Yesu akasema, “Bwana, nisaidie!” 26Yesu akajibu, “Si haki kuchu kua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.” 27Yule mwanamke akajibu, “Ndio, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yanayoan guka kutoka kwenye meza za mabwana wao.”

28Ndipo Yesu akamwambia, “Mama, imani yako ni kubwa! Na ufanyiwe kama unavyotaka.” Tangu wakati huo mtoto wake akapona.

Yesu Aponya Watu Wengi

29Yesu akaondoka mahali hapo akapita kando ya bahari ya Galilaya. Akapanda mlimani, akaketi huko . 30Umati mkubwa wa watu wakamjia wakiwaleta viwete, vilema, vipofu, viziwi na wen gine wengi, wakawaweka karibu yake; naye akawaponya. 31Watu wakashangaa walipoona bubu wakisema, vilema wakipona, viwete wakitembea na vipofu wakiona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.

Yesu Alisha Watu Elfu Nne

32Kisha Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, “Nina waonea huruma watu hawa kwa maana wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu sasa na hawana chakula. Sipendi kuwaaga wakiwa na njaa wasije wakazimia njiani.”

33Wanafunzi wake wakasema, “Tutapata wapi chakula cha kutosha kuwalisha watu hawa wote, nasi tuko nyikani?” 34Na Yesu akawauliza, “Mnayo mikate mingapi?” Wakamjibu, “Saba, na samaki wadogo wachache.” 35Yesu akaamuru watu wakae chini. 36Kisha akachukua ile mikate saba na wale samaki, akamshukuru Mungu, akavimega akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu. 37Wote wakala, wakashiba. Baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu saba. 38Idadi ya watu waliokula ilikuwa elfu nne bila kuhesabu wanawake na watoto.

39Baada ya kuwaaga watu, Yesu akaingia katika mashua akaenda sehemu za Magadani.