Mabakuli Saba Ya Ghadhabu Ya Mungu
1Kisha nikasikia sauti kuu kutoka Hekaluni ikiwaambia wale malaika saba, “Nendeni mkamwage duniani yale mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu.”
2Malaika wa kwanza akaenda akalimimina bakuli lake ardhini na madonda mabaya yenye maumivu makali yakawapata wote waliokuwa na alama ya yule mnyama na walioabudu sanamu yake.
3Malaika wa pili akamimina bakuli lake baharini , ikawa kama damu ya mtu aliyekufa na kila kiumbe hai kilichokuwa ndani ya bahari kikafa.
4Malaika wa tatu akamimina bakuli lake katika mito na chemchemi za maji, nazo zikageuka kuwa damu. 5Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, “Umefanya haki katika hukumu hizi uli zotoa, wewe uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu. 6Maana walimwaga damu ya watakatifu na manabii, na wewe umewapa damu wanywe, kama walivyostahili.” 7Nikasikia madhabahu ikiitikia, “Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, hukumu zako ni za kweli na haki.!”
Mungu Mwenyezi, hukumu zako ni za kweli na haki.!”
8Malaika wa nne akamimina bakuli lake kwenye jua nalo lika pewa nguvu za kuwachoma watu kwa moto wake mkali. 9Watu wakaun guzwa na moto huo nao wakalaani jina la Mungu aliyekuwa na uwezo juu ya maafa haya, wala hawakutubu na kumtukuza.
10Malaika wa tano akamimina bakuli lake kwenye kiti cha enzi cha yule mnyama, na ufalme wake ukawa gizani. Watu wakauma ndimi zao kwa uchungu 11wakamlaani Mungu wa mbinguni kwa mau mivu yao na madonda yao, wala hawakutubu kwa ajili ya matendo yao maovu.
12Malaika wa sita akamimina bakuli lake kwenye mto mkubwa wa Efrati, maji yake yakakauka ili kuwatayarishia njia wafalme kutoka mashariki. 13Nikaona roho wachafu waliofanana na chura wakitoka katika kinywa cha lile joka na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 14Hizo ni roho za pepo zitendazo miujiza. Nazo huwaendea wafalme wa ulim wengu wote na kuwakusanya tayari kwa vita, siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. 15“Sikiliza! Ninakuja kama mwizi! Amebarikiwa aliye macho, akiziweka tayari nguo zake ili asiende bila nguo na watu wakam wona uchi!” 16Kisha wakawakusanya wafalme pamoja mahali ambapo huitwa “Armageddoni” kwa Kiebrania.
17Malaika wa saba akamimina bakuli lake angani na sauti kuu ikatoka Hekaluni katika kile kiti cha enzi ikisema, “Imekwisha timia!” 18Kukawa na miali ya umeme, sauti, ngurumo za radi na tetemeko kuu la ardhi. Hapajawahi kuwa na tetemeko la ardhi kama hilo tangu mwanadamu kuwapo, kwani lilikuwa tetemeko kubwa ajabu.
19Ule mji mkuu uligawanywa katika sehemu tatu na miji yote ya mataifa ikaanguka. Mungu akakumbuka Babiloni kuu akainywesha kikombe cha divai ya hasira na ghadhabu yake. 20Kila kisiwa kikatoweka wala milima haikuonekana. 21Mvua kubwa ya mawe, mawe mazito karibu kilo hamsini, ikanyesha kutoka mbinguni ikawaangu kia wanadamu. Wanadamu wakamlaani Mungu kwa ajili ya maafa ya mvua ya mawe. Kwa maana lilikuwa ni pigo kuu la kutisha.