2 Wakorintho 4

Hazina Za Roho Kwenye Vyombo Vya Udongo

1Kwa hiyo tukiwa na huduma hii kwa rehema ya Mungu, hatu kati tamaa. 2Tumekataa njia za siri na za aibu. Hatutumii njia za udanganyifu, wala hatupotoshi neno la Mungu. Badala yake, tunaeleza neno la kweli wazi wazi na kujitambulisha kuwa wa kweli kwa dhamiri ya kila mtu mbele ya Mungu. 3Na hata kama Injili yetu imefichika, basi imefichika kwa wale wanaopotea. 4Kwa upande wao, mungu wa dunia hii ametia giza akili za wasioamini, ili wasione mwanga wa Injili ya utukufu wa Kristo, ambaye ana sura ya Mungu. 5Kwa maana hatujihubiri sisi wenyewe ila tunamhu biri Yesu Kristo kuwa ni Bwana, na sisi ni watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. 6Kwa kuwa ni Mungu aliyesema, “Nuru iangaze katika giza,” ambaye ameangaza mioyoni mwetu kutupatia nuru ya ufahamu wa utukufu wa Mungu ung’aao katika uso wa Kristo.

7Hata hivyo tunayo hazina hii katika vyombo vya udongo, ili kuonyesha kwamba uwezo huu wa ajabu unatoka kwa Mungu, na si kutoka kwetu. 8Tumegandamizwa kila upande, lakini hatujashindwa. Tumetatanishwa lakini hatukati tamaa; 9tumeteswa lakini hatuku achwa upweke; tumetupwa chini lakini hatujateketezwa. 10Tuna chukua katika mwili wetu kifo cha Yesu wakati wote ili uhai wa Yesu uweze kudhihirika katika miili yetu. 11Kwa maana sisi tunaoishi, maisha yetu yako katika hatari ya kifo wakati wote kwa ajili ya Yesu ili uhai wake uweze kuonekana katika miili yetu ya mauti. 12Kwa hiyo, mauti inatuandama wakati wote, bali uzima unafanya kazi ndani yenu. 13Maandiko yanasema, “Niliamini, kwa hiyo nimesema.” Sisi pia tunaamini, kwa hiyo tunasema. 14Kwa maana tunajua ya kuwa aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua na sisi pamoja na Yesu na kutufikisha sisi na ninyi mbele zake. 15Haya yote ni kwa ajili yenu, ili kwa kadiri neema ya Mungu inavyowafi kia watu wengi zaidi, wote watoe shukrani kwa utukufu wa Mungu.

16Kwa hiyo, hatukati tamaa. Ingawa miili yetu inachakaa, utu wetu wa ndani unafanywa upya kila siku. 17Maana hii dhiki yetu nyepesi na ya muda mfupi inatutayarisha kwa ajili ya utukufu wa uzima wa milele unaozidi sana matatizo haya. 18Kwa maana hatuweki mawazo yetu kwenye vitu vinavyoonekana bali kwenye vitu visivyoonekana. Maana vile vinavyoonekana ni vya muda mfupi, lakini vile visivyoonekana vinadumu milele.